Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema bei za treni za mchongoko zitakuwa Tsh. 100,000 hadi 120,000 kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ambapo treni hizo zitakuwa ni express ambazo hazitosimama kila kituo bali kutoka Dar es salaam zitasimama Morogoro kisha Dodoma .
Akiongea Jijini Dar es salama leo June 12,2024, Kadogosa amesema “LATRA wametangaza nauli za daraja za kawaida lakini tutakuwa na treni za aina tatu, treni za kawaida ambazo zinasimama kote, tutakuwa na treni za express ambayo ikitoka hapa inasimama Morogoro, Morogoro - Dodoma lakini pia tutakuwa na treni nyingine ambayo ni high class zaidi zile za mchongoko tumeshaanza kuifanyia majaribio lakini June 16,2024 tutapokea nyingine mbili”
“Mule ndani kuna class mbili economy na business lakini ile nyingine kuna business lakini pia kuna Royal business kuna sehemu wanakaa Watu 48 tu na nyingine wanakaa chini ya hao Watu, business tutaenda kwa Tsh. elfu 70, katika ile ya mchongoko Royal tutaenda kwa Tsh. 120000 na business ya kawaida laki 1 na itakuwa express”
“Tunafanya hivyo Ndugu Waandishi wa Habari naomba hili mliweke vizuri tunajaribu ku-accomodate Watu wote, kuna zile ambazo mmetangaziwa, najua Watu watalalamika lakini hatuwezi kuwa na mentality ileile”
Itakumbukwa hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilitangaza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA kuhusu nauli za abiria wa daraja la kawaida kwa Treni ya Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora baada ya kufanyia kazi maombi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na maoni ya Wadau wengine ambapo Dar es salaam hadi Morogoro (KM 192) nauli ni Tsh. 13000 na Dar es salaam hadi Dodoma (KM 444) nauli ni Tsh. 31000.
إرسال تعليق