URUSI YASAINI MKATABA

 URUSI: Rais #VladimirPutin amesaini amri inayoruhusu kukamatwa kwa mali za Raia wa Marekani na Kampuni zao zilizopo Urusi ikiwa ni sehemu ya fidia ya Vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya #Moscow


Amri hiyo ya Putin itazipa Kampuni za Urusi, Mashirika na Watu binafsi walioathiriwa na vikwazo, haki ya kuomba fidia kwa Serikali ya Urusi kisha Serikali itatumia mali za Marekani kuwalipa


Nchi za Magharibi zilizuia mali za Urusi zenye thamani ya Dola Bilioni 300 (Tsh. Trilioni 776), baada ya Moscow kupeleka Wanajeshi kuivamia #Ukraine Februari 2022


Bunge la Marekani lilipitisha Sheria ya REPO inayoruhusu Utawala wa Rais #JoeBiden kuchukua mali za Urusi zinazoshikiliwa katika Benki za Marekani ili kuisaidia Ukraine

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم