🚨RAMADHAN SINGANO ‘MESSI’ ameshinda kesi yake dhidi ya TP Mazembe ambayo ilikuwa kwenye korido za FIFA ambapo nyota huyo aliyesajiliwa Lubumbashi mwaka 2019 alipeleka kesi FIFA baada ya mkataba wake kuvunjwa kinyume na utaratibu huku akidai mishahara yake, malimbikizi na gharama za ziada ambapo Mazembe walipaswa kumlipa dola 585,000 za Kimarekani sawa na BILLION 1.5 za Kibongo.
Tarehe ya malipo ilikuwa ni Agosti 15,2024 ambapo taarifa ni kuwa Mazembe ni kweli walilipa mzigo huo kwenye akaunti ya Ramadhan Yahaya Singano ya benki ya NMB kiasi cha BILLION 1.5 kupitia tawi la Bank House jijini Dar Es Salaam, ambapo baada ya malipo hayo wakafungua shauri Mahakama Kuu jijini Dar Es Salaam wakitaka Akaunti ya Singano ifungiwe ili asiweze kutoa fedha hizo.
Sababu kubwa ya Mazembe kuomba Mahakama ya Tanzania ifungie akaunti ya Singano asitoe mzigo ni kuwa wanadai Singano alikuwa na kesi huko Katanga, Congo ambapo Mazembe walifungua wakidai Nyota huyo alifanya udanganyifu na Mazembe walishinda huku Mchezaji akipaswa kuwalipa kiasi cha dola 685,000 za Kimarekani.
Mchuano ni mkali sana kati ya Singano na TP Mazembe ila mpaka hapa naona Katumbi kuna mchezo anaucheza, yani amemlipa Mchezaji kama FIFA walivyoagiza halafu anazitaka fedha zake kwa style hiyo ila mpaka sasa Mahakama ya Tanzania imetupilia mbali ombi hilo la Mazembe.
[Taarifa kwa msaada wa gazeti la THE CITZEN]
Post a Comment