STEPHEN AZIZ KI ana offer mbili kutoka Al Ahly na Orlando Pirates, amewapa Yanga unafuu wa offer ili aweze kusaini kwao na mahitaji yake kutoka kwa vyanzo vyangu anahitaji kiasi cha dola 500,000 ili aweze kusaini ikiwa ni sawa na BILLION 1.2 za Kitanzania.
Mpaka hivi sasa Wananchi hawana kiasi hicho na klabu kwa mujibu wa vyanzo imejipiga mpaka Dola 350,000 za Kimarekani wapo tayari kumpa ila Aziz ameshikilia zifike 500,000 ili asaini, jitihada zinaendelea ila kinachohitajika ni huo mzigo.
Mpaka hivi sasa Aziz hajasaini KARATASI yoyote ndani ya Jangwani. Source Farhan kihamu Jr via Twitter
Post a Comment