Dondoo za soka Ulaya

 


Kiungo wa kati wa Ujerumani Jamal Musiala amekataa kandarasi mpya katika klabu ya Bayern Munich, akilenga kuhamia Ligi ya Premia msimu wa joto, huku Manchester City na Liverpool wakiongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Star)

Kocha Thomas Tuchel huenda akafutwa kazi ikiwa Bayern Munich itapoteza mchezo wao wa mkondo wa 16 bora wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Lazio Jumanne. (Sky Sports )

Kocha wa Manchester United Erik ten Hag anamfuatilia mlinzi wa Girona Mhispania Miguel Gutierrez, 22 kabla ya dirisha la usajili la kiangazi. (Sun )



Liverpool wamezidisha nia yao ya kutaka kumnunua kocha mkuu wa Sporting Lisbon Ruben Amorim, lakini kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso anasalia kuwa mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Jurgen Klopp. (Mirror)

Matumaini ya Barcelona kumteua mkufunzi wa Brighton Roberto de Zerbi msimu wa joto yametatizwa na kukataa kwa Seagulls kufanya mazungumzo kuhusu kipengele cha kuachiwa cha euro 15m (£12.8m) cha Muitaliano huyo. (Sport - kwa Kihispania)

Klabu ya Barcelona imefanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Ujerumani Hansi Flick kuhusu kurithi mikoba ya Xavi. (Florian Plettenberg)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe amekutana na Luis Enrique ili kutatua mvutano unaotokana na kocha mkuu wa Uhispania kumbadilisha mchezaji huyo wa miaka 25 katika michezo ya hivi karibuni. (ESPN)


Fulham, Everton, West Ham na Wolves wanamfuatilia winga wa Galatasaray mwenye umri wa miaka 31 wa Ivory Coast Wilfried Zaha. (Ekrem Konur)

Arsenal na Manchester City wanashindana kumsajili mchezaji wa Fiorentina mwenye umri wa miaka 19 na beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Italia chini ya umri wa miaka 21 Michael Kayode. (Fichajes )

Barcelona itaweka kipaumbele katika kuwauza winga wa Brazil Raphinha, 27, na mlinzi wa Ufaransa Jules Kounde, 25, msimu wa joto. (Sport)

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post